yang2020 ии artificialintelligence искусственныйинтеллект solidstatelife technology machinelearning humor tech design blockchain innovation dnc illustrator bigdata iot crypto blm lidertoken python programming art mlm ctl invest robotics sgp чертановобаскет
Picha hii inamuonesha baba akiwa na binti yake mwenye miaka 6.Binti huyu alizaliwa na matatizo ya kusikia (kiziwi) kwenye sikio lake la kushoto.Kutokana na hali hii,madaktari walimfungia mtoto huyu kifaa maalumu kinachomuwezesha kusikia (cochlear implant) kwenye sikio hili.Baada ya kufanyika kwa tukio hili,shida moja tena ilijitokeza ambapo mtoto alipoteza kabisa hali ya kujiamini akawa hana furaha muda wote kutokana na kujiona kuwa yupo tofauti na watoto wengine.
Jambo hili lilimfanya baba yake abadili style ya kunyoa nywele ndipo akaanza kunyoa upara na sehemu ya kushoto ya sikio lake akaichora tatoo inayofanana na kifaa anachovaa mwanae (cochlear tatoo).Kwa miaka miwili sasa,mtoto huyu amekuwa akiishi kwa furaha,anajiamini na amechukulia kifaa anachovaa kama style tu sababu baba yake anacho pia.Wanaume wa kitanzania tunayaweza haya mambo au tukishazalisha ndiyo mwisho wa malezi
#AI
Kumbemenda mtoto ni nadharia inayomaanisha kudhoofika kwa afya ya mtoto wakati wa siku za mwanzo kabisa za matumizi ya ziwa la mama yake.Hudhaniwa kutokana na mama kushiriki tendo la ndoa na mmewe au hata kutoka nje ya ndoa wakati bado ananyonyesha.Imani hii huenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa shahawa au mbegu za kiume zinazomwagwa wakati wa tendo la ndoa huingia na kuchanganyikana na maziwa ya mama ambayo baadae hunyonywa na mtoto hivyo kusababisha hali ya kubemendwa kwa mtoto
.
.
UKWELI NI UPI?
Haya ni madai ya uongo kwa 100% na hayana hata chembe ya ukweli.Shahawa/manii au hata mbegu za kiume zinazotolewa wakati wa tendo la ndoa huishia safari yake kwenye tumbo la uzazi na huharibiwa huko.Haziwezi kuingia kwenye mfumo wa mzunguko wa damu mwilini hivyo hakuna namna zitaingilia uzalishwaji wa maziwa ya mama
.
.
LINI MWANAMKE AFANYE MAPENZI BAADA YA KUJIFUNGUA?
Tendo hili mara nyingi hushauriwa lifanyike wiki 6 baada ya kujifungua.Linaweza pia kufanyika hata baada ya wiki 4 ikiwa tu uchafu na majimaji yenye damu yanayotolewa na mama kupitia uke yatakoma.Tendo hili hutegemea utayari wa mama,uwezo wake katika kulihimili na kasi ya kupona kwa vidonda na mipasuko aliyoipata wakati wa kujifungua.
.
.
MUHIMU
Kubemendwa kwa mtoto hakuna uhusiano wowote na kufanya mapenzi.Ukiona afya ya mwanao inadhoofika ni lazima atakuwa na matatizo ya kiafya,au hata hapati matunzo na virutubisho vya kutosha.Inaweza ikawa sababu hapati maziwa ya mama ya kutosha,hanyonyi vizuri,kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema hasa kabla ya miezi 6 ya mwanzo,homa za mara kwa mara,nimonia,UTI pamoja na matatizo mengine mengi.Ni vyema akapelekwa hospitalini mapema ili asaidiwe kuliko kuendelea na dhana POTOFU ya kusingizia kuwa tendo la ndoa ndiyo chanzo.Naomba kuwasilisha!
#AI
Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kupelekea mtu awe anateseka kila mara kwa kupata choo kigumu.Pamoja na ukweli huu,sababu hizi 6 ndizo huchukua sehemu kubwa ya tatizo hili ambazo ni
1.Kutokunywa maji mengi
2.Kutokula matunda
3.Matumizi makubwa ya supplements (virutubisho) zenye madini mengi ya chuma na calcium
4.Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za bakteria,hasa yasiyofuata ushauri wa madaktari au wafamasia
5.Ulaji mwingi wa bidhaa za maziwa (dairy products)
6.Kutokufanya mazoezi
Kama unakabiliwa na tatizo hili,chunguza kwa umakini sababu hizi sita.Kama unadhani mambo haya yote hayahusiki kwenye tatizo lako basi fika hospitalini haraka usaidiwe kwani choo kigumu kinaweza kuwa ni ishara ya uwepo au dalili ya awali inayoashiria uwepo wa matatizo mengine makubwa ya kiafya.Tafuta msaada wa haraka!
#AI