sisinimashahiditu hallaywsmm enjoysoccer maajabu mkutano_mkubwa stormmichezo uncle yangascvasvita sisinisokaburudaniinaendelea
Mapema tu Mganda Juma Balinya ameanza kuteka mioyo ya mashabiki wa Yanga kutokana na makali anayoonyesha
:
Baada ya Yanga kumuuza aliyekuwa mshambuliaji tegemeo Heritier Makambo, baadhi ya mashabiki walipata hofu
'
Akiwa tayari ameifungia Yanga mabao mawili kwenye michezo ya kirafiki, Balinya ameonyesha huenda akawasahaulisha kabisa mashabiki kuhusu Makambo
:
Ingawa bado ni mapema sana, lakini Balinya ameanza kujijengea ufalme kwenye kikosi cha Yanga
:
Wakati Balinya akianza kuonyesha makali, kazi itakuwa kwa washambuliaji wengine Sadney Urikhob aliyetua hivi karibuni na Maybin Kalengo aliyeanza kwa kasi kabla ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu
:
Sadney alichelewa kuripoti kambini, pengine atahitaji muda zaidi ya kujifua
:
Lakini wengi wana matumaini makubwa kwake kutokana na umahiri wake katika kuzifumania nyavu
#sisiNiMashahidiTu
#hallaywsmm
WILFRED Kidao, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao wa 2019/20 ameshapatikana na kinachosubiriwa ni kusainiwa kwa mkataba.
:
Kidao ametoa taarifa hiyo wakati akijibu swali la #ywsmm_tz kupitia pag yetu ya twitter ambako wadau mbalimbali wa soka wanauliza maswali kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa shirikisho hilo la TFF, utaratibu alioamua kuufanya mara moja kila wiki
#sisiNiMashahidiTu
#hallaywsmm
Mchezaji wa timu ya Yanga kutoka nchini Namibia Sadney Urikhob anatarajiwa kuwasili hapa nchini hapo kesho tayari kujiunga na kambi ya timu hiyo mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya uongozi wa klabu zinaeleza kuwa Urikhob ameshindwa kuwasili kwa wakati kwa kuwa alikuwa ana matatizo binafsi katika familia yake.
#sisiNiMashahidiTu
#hallaywsmm